Shabiki aliyemuita Kipa nyani afungiwa

Shabiki aliyemuita Kipa nyani afungiwa

Shabiki anayedaiwa kufanya ubaguzi wa rangi kwa ‘golikipa’ wa ‘klabu’ ya #ACMilan, #MikeMaignan amefungiwa kutohudhuria katika viwanja vyote vya soka vya nchini Italia kwa miaka mitano.

Inaelezwa kuwa mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 46 anatuhumiwa kumzomea mlinda mlango mara 12 akimwita ‘Nyani’ wakati wa ‘mechi’ ya Series A iliyochezwa siku ya Jumamosi kwenye mji wa #Udine.

Hata hivyo Jeshi la Polisi nchini humo wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kupitia Camera za CCTV na mitandao ya kijamii ili kujaribu kuwatambua watu wengine ambao huenda walihusika katika tukio hilo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags