Senegal yazuia upatikanaji wa intaneti

Senegal yazuia upatikanaji wa intaneti

Serikali nchini Senegal imezuia upatikanaji wa intaneti kwenye simu ili kusimamisha ueneaji wa taarifa zinazoweza kuleta machafuko zaidi.

Hii ni baada ya wafuasi wa Ousmane Sonko kufanya ghasia kutokana na hukumu aliopatiwa kiongozi huyo wa upinzani.

Sonko ambaye ni mwanasiasa mpinzani na mkosoaji wa serikali, amehukumiwa jela miaka miwili kwa kukutwa na hatia ya kumbaka na kumpa vitisho vya kifo binti aliyekuwa akifanya kazi katika sehemu ya kutoa huduma za masaji

Sambamba na hayo shirika la msalaba mwekundu la hiyo limesema watu zaidi ya 350 wamejeruhiwa huku 16 wamefariki katika machafuko hayo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post