Schwarzenegger aachiwa

Schwarzenegger aachiwa

Muigizaji wa filamu kutoka Marekani Arnold Schwarzenegger, ameruhusiwa kupiga mnada saa yake ya gharama nchini Austria, baada ya kutolewa kizuizini katika uwanja wa ndege wa Munich nchini Ujerumani, baada ya kukaa hapo kwa muda.

Arnold mwenye miaka 76, alikamatwa kwa tuhuma za kukwepa kodi baada ya kushindwa kuonesha saa hiyo ya thamani kubwa akiwa uwanja wa ndege wakati alipokuwa akielekea Austria kwa ajili ya kuiuza, lakini baadaye alilazimika kuilipia kodi na kuruhusiwa kuendelea na safari.

Kwa sheria za Umoja wa Ulaya mtu yeyote anayewasili na pesa taslimu au vitu vya thamani vinavyozidi euro 10,000 anatakiwa kuweka wazi kwa ajili ya kuvilipia kodi na mitandao mingi haijasema saa hiyo ni ya thamani gani.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags