Saudi Arabia kuandaa kombe la dunia 2034

Saudi Arabia kuandaa kombe la dunia 2034

Imeripotiwa kuwa nchini #SaudiArabia, wataandaa Kombe la Dunia la 2034, baada ya #Australia kujiondoa kwenye kinyang'anyiro cha kuandaa mashindano hayo.

Inaelezwa kuwa nchi hiyo ilipeleka maombi #FIFA ya kuandaa Kombe la Dunia la mwaka 2034, ikiwa ni sehemu ya mpango wa mwanamfalme Mohammed bin Salman, kufanya mapinduzi ya kibiashara na ‘kisoka’ kupitia mradi wa Vision 2030.

Hata hivyo, ‘ripoti’ kutoka nchini #Australia zinasema kuwa, Taifa hilo lilifanya uamuzi wa kujitoa kuandaa michuano hiyo siku ya leo Jumanne Oktoba, 31.

Kufuatia hatua hiyo, Saudi Arabia inasalia katika kuandaa michuano hiyo ya kimataifa, hivyo wanatarajiwa kutangazwa rasmi kuwa wenyeji wa Kombe la Dunia kwa mwaka 2034.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags