Baada ya watumiaji wa simu za Iphone kushindwa kupakuwa (download) application mbalimbali nje ya App Store, hatimaye kampuni ya simu hizo imefanya mabadiliko.
Kampuni ya Apple imeanza kuruhusu watumiaji wake ku-download application kwenye website nyingine ikiwemo Google, katika masasisho ya ios 17.4.
Ruhusa hii imeanza kwa watumiaji wa Ulaya, hii inamaana kuwa, watumiaji wa iphone bara la Ulaya watakuwa na uwezo wa kupakua application nje ya App Store.
Ikumbukwe kuwa jambo hili siyo geni kwa watumiaji wa android, kwani wao huweza kudownload application kutoka sehemu mbalimbali.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi
Leave a Reply