Sancho aondolewa kikosi cha kwanza

Sancho aondolewa kikosi cha kwanza

‘Winga’ wa ‘klabu’ ya Uingereza ya Manchester United, Jadon Sancho ameondolewa kwenye kikosi cha kwanza na badala yake atafanya mazoezi na kikosi cha vijana cha ‘timu’ hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika ‘timu’ hiyo imeeleza kuwa Sancho atasalia kwenye ‘programu’ ya mazoezi ya kibinafsi mbali na kikosi cha kwanza huku akisubiri suluhu juu ya suala lake la kinidhamu.

Ikumbukwe sekeseke hilo limetokea baada ya nyota huyo kumjibu wazi wazi ‘kocha’ Eric Ten Hag licha ya kutomtaja jina na kudai kuwa ni muongo baada ya ‘Kocha’ kusema hakumpanga mchezaji huyo kwa sababu hakuwa na kiwango kizuri mazoezini.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags