Samsung Afrika Mashariki yakutana na wadau kuimarisha mahusiano

Samsung Afrika Mashariki yakutana na wadau kuimarisha mahusiano

Kampuni ya Kielektroniki ya Samsung Afrika Mashariki imekutana na wadau wake wa kibiashara Jijini Dar es Salaam wakiwemo wafanyabiashara na wasambazaji wa bidhaa zake zote kutoka pande zote za nchi ya Tanzania kwa lengo la kuimarisha mahusiano

Mkutano huo ambao uliandaliwa na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo Afrika Mashariki, Tae Sun Lee, ulifanyika jana na kuhudhuliwa na wafanyabiashara zaidi ya 100 waliokutana na kujadili mahitaji ya soko na jinsi gani kwa pamoja wanaweza kukuza soko la Samsung nchini Tanzania.

Akizungumza katika mkutano huo, Lee amesema lengo kuu la mkutano huo ni kuwaleta pamoja wadau wakuu wa bidhaa za Samsung wakiwemo wasambazaji na wafanyabishara ili kuhakikisha matumizi bora zaidi yanatolewa kwa mtumiaji wa bidhaa za kampuni hiyo.

Amesema kampuni ya Samsung inaendelea kuamini kuwa maendeleo ya kiteknolojia ndio kichocheo kikuu cha biashara ya bidhaa zake ulimwenguni.

“Kampuni ya Samsung itaendelea kuimalisha mahusiano yetu na washirika wetu wakiwemo wasambazaji wote kutoka pande zote za Tanzania na ukanda mzima wa Afrika Mashariki,” amesema

Lee amesema kuwa Kampuni ya Samsung itaendelea kuhakikisha bidhaa zote zinazotengenezwa na Kampuni hiyo zinaendelea kuwa zenye ubora wa hali ya juu ili kumpa furaha na faraja mtumiaji wake.

Ameongezea kuwa mkakati mkubwa wa kampuni hiyo ni kuendelea kuona bidhaa zake za kielektroniki zinaendelea kuwa bidhaa pendwa kabisa katika soko la Afrika.

"Kama Samsung tunasisitiza kuwa tutaendelea kuwa na sauti moja pale tunapoweka mikakati yetu ili tuweze kwenda mbele. Mienendo yetu ya soko inaendelea kubadilika na pia tunaona haja ya kurekebisha katika maeneo mbali mbali ili kukidhi mahitaji ya wadau,” amsema Lee

Katika mkutano huo, Kampuni ya simu ya Tigo walianzisha mashirikiano na Samsung ikiwa ni mpango kabambe wa kumuwezesha mteja anayetumia Samsung ‘Smart TV’ kuweza kupata kifaa cha kumuwezesha kutumia intanet kwenye luninga yake cha Mi-Fi kutoka Tigo.

Katika makubaliano hayo, mteja atakaye atanunua luninga ya Samsung smart katika kipindi cha ofa ataweza kupata kifaa hicho cha MiFi kutoka Kampuni yaTigo kikiwa na kifurushi cha kuanzia ili kumuwezesha kujiunga na mtandao wa intanet katika luninga yake

Akizungumzia mashirikiano hayo, Ofisa Mkuu (Mikakati na Ubunifu) wa Kampuni ya Tigo, David Umoh amesema: “Kama Tigo, kupitia teknolojia tunalenga kufanya maisha ya Mtanzania kuwa bora zaidi ndiyo maana tumeamua kushirikiana na Kampuni ya Samsung katika kuhakikisha kila mteja atakaye nunua Smart TV ya Samsung anapata kifaa cha intanet cha MiFi kutoka Tigo.”

Umoh ameongezea kuwa kampuni ya Samsung imekuwa mmoja wa washirika wao wakuu nchini Tanzania na amesisitiza kuwa wataendelea kufanya kazi pamoja ikiwa ni katika mipango chanya ya kuhakikisha maisha ya mtanzania yanakuwa bora zaidi.

Zaidi ya hayo, Kampuni ya kielectroniki ya Samsung iliunganisha pamoja kitengo chake cha simu pamoja na kile cha watumiaji wa bidhaa mbali mbali kuwa kitengo kimoja cha DX.

Lengo kuu la kuweza kuwa na kitengo kimoja ni kumuwezesha mtumiaji wa bidhaa za Samsung kupata huduma zote sehemu moja.

Hata hivyo Kampuni ya Samsung imetanabahisha kuwa wataendelea kutengeneza bidhaa mbalimbali na kutoa huduma bora zaidi ili kuendela kudumisha mahusiano yao na watumiaji.

Katika mkutano huo, bidhaa mbalimbali za Kampuni ya Samsung za mwaka 2022 zimeonyeshwa zikiwemo simu ambapo bidhaa hizo zikilenga kikazi cha millennia, Z.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags