Safia Jongo: Ukiingia polisi bure, na kutoka ni bure

Safia Jongo: Ukiingia polisi bure, na kutoka ni bure

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, Safia Jongo amepiga marufuku tabia ya baadhi ya Askari kuomba rushwa pale ambapo Mtuhumiwa anapokamatwa na kupewa dhamana na Ndugu zake kwa kumtaka atoe chochote.

Akiongea na Wakazi wa Kata ya Kamoge Wilayani Bukombe Mkoani Geita Katika ziara aliyofanya Mkuu wa Mkoa wa Geita Martin Shigella, Jongo amesema ni marufuku Mwananchi kutoa kitu chochote kwa Askari endapo Mtuhumiwa atapewa dhamana na Ndugu zake kwa kutimiza Masharti.

"Jamani ehee kuingia Polisi bure kutoka hela hili jambo marufuku mbele ya Uongozi wangu Mimi Bibi yenu, ukiingia Polisi bure kutoka bure, wewe ukitoa hela umetoa rushwa na sitakubali nawaachia namba yangu ya simu mniambie huyo Askari anayedai hela kutoka ndani ya kituo cha Polisi Mimi sasa hivi nimehama kwenye Ubibi nitakuwa Shangazi” amesema RPC

Aidha amesema kuwa baadhi ya Askari wamekuwa wakilichafua Jeshi la Polisi huku akiahidi endapo watagundulika atawachukulia hatua za Kisheria huku akiwataka Wananchi kutoa taarifa mapema kwa atakayeendelea kufanya hivyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post