Sababu za wajawazito kufanya mapenzi kila siku

Sababu za wajawazito kufanya mapenzi kila siku

Haya haya kumekucha watu wetu wa nguvu wa Mwananchi Scoop, kila siku asubuhi tunakusogezea mada hatari kuhusiana na mahusiano na hapa tukizungumza mahusiano kwa ujumla yaani ndoa na uchumba.

Kubeba ujauzito sio jambo dogo kukibeba kiumbe tumboni kwa miezi tisa kunaweza kuleta msongo wa mawazo Zipo njia mbalimbali zinazoweza kumpunguzia mwanamke mjamzito msongo wa mawazo katika kipindi cha ujauzito kama best sex ambayo huwezi kuipata katika kipindi kingine cha maisha na inasiadia kuimarisha misuli katika njia za uzazi hata baada ya kujifungua.

Wanawake wengi na wanaume kwa ujumla huwa wanajiuliza ni kwanini mama mjamzito akiwa katika hali hiyo anakuwa na hamu sana ya kufanya tendo la ndoa kila siku basi leo nimekuja kukujuza Zaid. Na hizi ni sababu zinazomsaidia yeye kiafya.

  • Husaidia mjamzito kupata usingizi mnono.
    Mjamzito anakumbwa na mambo mbalimbali yanayoweza kumnyima usingizi kama maumivu kwa mbali kwenye uti wa mgongo, kukojoa mara kwa mara, masaa ya kulala kupungua/kuonekana mafupi fetus anavyozidi kukua katika mfuko wa uzazi. Kufanya tendo la ndoa katika kipindi cha ujauzito kunamsaidia mwanamke kufika kileleni na hivyo kupata usingizi mnono kwani huisi kupungukiwa na mzigo mzit

 

  • Husaidia presha kushuka.
    katika kipindi cha ujauzito inasidia kushusha presha ya damu Oxytocin, love homoni inayozalishwa kwa wingi mtu akifanya mapenzi inasaidia kupunguza kama sio kuondoa kabisa msongo wa mawazo na kuhakikisha presha iko katika hali ya kawaida ya mwili.

 

  • Kupunguza maumivu
    Homoni kama oestrogen, prolactin na progesterone zinasaidia damu kupita kwa wingi katika maeneo ya nyonga,na hata kwenye uke uongeza hisia na utelezi.

 

  • Inasaidia mwanamke kuwa karibu zaidi na mumewe kwenye kipindi hiki.
    Bondi kati ya mume na mke inaendela kuwepo kwani wanaweza kuendelea kufanya mapenzi kwenye kipindi hiki cha ujauzito, Wanawake wanakuwa na hali isiyo ya kawaida na mara nyingi huwa na hasira wanatakiwa kuangaliwa kwa umakini Oxytocin inamfanya mwanamke awe anajali,na kuamini kuwa mpenzi wake anamjali.

Ooohooooh! Nathani mtakuwa mmejifunza kitu kupitia mada hii, usiache kufuatilia mitandao yetu ya kijamii kwa mada kama hizi na nyinginezo nyingi @Mwananchiscoop






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags