Sababu ya kifo cha Darius Morris yatajwa

Sababu ya kifo cha Darius Morris yatajwa

Mchezaji  NBA Darius Morris anatajwa kufariki kwa ugonjwa wa moyo, huku matumizi ya dawa za kulevya na pombe yakitajwa kama chanzo, mchunguzi wa afya wa Kaunti ya Los Angeles alithibitisha kwa ABC 7 na TMZ Sports jana Jumamosi juni 15, 2024, huku akitaja  dawa zinazoweza kuchangia katika kifo cha aina hiyo ni pamoja na ethanol, kokeini, na haidrokodoni.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 aliaga dunia ghafla mnamo Mei 4 mwaka huu, hali iliyoshtua ulimwengu wa mpira wa kikapu.

Wakati huo, familia yake ilithibitisha kifo chake katika taarifa kupitia tovuti ya TMZ huku ikiomba faragha. "Kwa masikitiko makubwa tunatangaza kufariki kwa mtoto wetu mpendwa, Darius Aaron Morris," taarifa hiyo ilisema. "Wakati huu wa mapito, familia yake inaomba kuheshimu matakwa yao ya faragha."

Morris alijipatia jina kwa mara ya kwanza akiwa kama mchezaji wa Chuo Kikuu cha Michigan, ambapo aliisaidia timu yake kushindana katika mashindano ya mpira wa kikapu ya wanaume ya NCAA Division 1. Morris alianza kazi yake rasmi kwenye timu ya Los Angeles Lakers, ambao walimchagua kutoka chuoni mwaka 2011.

Baada ya kutumikia misimu kadhaa na timu hiyo, alijiunga na timu nyingine nne kabla ya kustaafu kazi yake ya kucheza mpira wa kikapu. Kwa muda wake aliokuwepo kwenye ligi ya NBA, alipata wastani wa pointi 3.3 kwa kila mchezo pamoja na asisti 1.4 na rebound 1.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags