Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Duniani 'WBF' limeweka wazi suala la bondia Hassan Mwakinyo kuvuliwa mkanda wa ubingwa wa WBF Intercontinental na kupelekea kupoteza pambano lenye malipo ya zaidi Euro 30,000 sawa na Sh. 78 Milioni 78 za Kitanzania.
WBF kupitia mwakilishi mkazi, Chatta Michael ametoa taarifa hiyo ambayo inaeleza sababu kubwa ya Mwakinyo kuvuliwa mkanda ni kutokana na kushindwa kutetea mkanda huo katika kipindi cha miezi mitatu kwa mujibu wa makubaliano yao ili kutoa nafasi kwake ya kwenda kupigania mkanda wa ubingwa wa Dunia wa WBF ambao angeweza kuingiza kiasi cha Euro 30,000 ikiwa sawa na Sh milioni 78 za kibongo.
WBF haikushia hapo kwani imewekazi kwamba iliweza fanya mawasiliano na management ya Mwakinyo na kuwaeleza juu ya bondia huyo kwenda kupigania mkanda wa Ubingwa wa ABU huku akijua kufanya hivyo ni kosa la kujivua ubingwa lakini WBF walijibiwa mkanda hao wa Intercontinental ni mdogo sana kuwa malengo yao yalikuwa kwenye mkanda wa ABU.
Kwa upande wa bondia Ibrahim Class, WBF imesema kuwa sababu kubwa ya bondia huyo kuvuliwa ubingwa ni kutokana na mwenyewe kutokuwa na mipango ya kutetea mkanda wake wa WBF Intercontinental kabla ya kumvua ubingwa huo na kupelekea kukosa sifa za kuwania mkanda wa ubingwa wa Dunia wa WBF.
Leave a Reply