Sababu akaunti nyingi za Whatsapp kufungiwa

Sababu akaunti nyingi za Whatsapp kufungiwa

Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa watumiaji wengi wa WhatsApp yakihusisha akaunti zao za mtandao huo kufungiwa bila ya wao kujua chanzo. @mwananchiscoop tunakujuza sababu zitakazopelekea akauti yako ifungiwe.

•Laini yako 'kublockiwa' na watu wengi
WhatsApp na mitandao mingi ya kijamii imetoa option za kuwaripoti na ku-block watu wote ambao wanatumiwa vitu tofauti na walivyo tarajia hivyo basi mtandao huo ukiona umeblockiwa na watu zaidi ya 10 basi utachukua jukumu la kufungia akaunti yako.

•Kutuma ujumbe (text) nyingi kwa watu ambao huna desturi ya kuwasiliana nao mara kwa mara
Sababu nyingine ya anaunti nyingi kufungiwa ni ku-forward ujumbe (text) nyingi kwa watu ambao huna desturi ya kuwasiliana nao mara kwa mara, maofisa wa WhatsApp wanaweza kudhani kuwa umeibiwa au kupoteza simu hivyo wataifungia akaunti hiyo kwa muda.

•Kutuma mafaili yenye utata
Akaunti yako ya WhatsApp inaweza kufungiwa kutokana na kutuma 'mafaili' ambayo yana utata hivyo basi akaunti yako inaweza kufungiwa kwa lengo la kuimarisha usalama wa mahali au taifa ulilopo.

•Kujiunga katika ma-group mengi ndani ya muda mfupi
Kujiunga katika ma-group mengi kunaweza kuwa jambo la kawaida lakini inaweza kutiliwa shaka na Whatsapp kuwa huwenda ikawa kuna mtu anatumia WhatsApp yako bila ya idhini yako.

•Kutumia matoleo mapya ya WhatsApp mfano, "WhatsApp Plus" au "GB WhatsApp"
Kwa mujibu wa ‘Wati blogu’ imeeleza kuwa kuna baadhi ya simu bado hazijaidhinishwa kutumia matoleo hayo mapya ya Whatsapp mfano simu za ‘Android’ hivyo basi watendaji wa mtandao huo wakigundua hilo wataifungia akaunti yako mara moja, na kuizuia namba yako kujiunga na mtandao huo.

•Kutumiwa taarifa binafsi za watu waliopo kwenye WhatsApp yako
Maofisa wa mtandao huo siku zote hutilia maanani taarifa binafsi za watumiaji wake hivyo basi haijalishi nia yako itakua nini kama ikigundua umetumiwa taarifa nyingi mfano, stika, namba za simu basi itachukua jukumu la kufungia akaunti yako.

•Ukiukwaji wa sheria na masharti ya WhatsApp
Mbali na kutuma ujumbe wa kero, vitisho, chuki, ubaguzi na nyinginezo, watumiaji wanaokiuka masharti ya huduma ya WhatsApp pia akaunti zao zitafungiwa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post