Ruto aagiza mchungaji Mackenzie ashtakiwe

Ruto aagiza mchungaji Mackenzie ashtakiwe

Rais William Ruto ametoa wito wa kushtakiwa kwa mchungaji Paul Mackenzie kuhusiana na vifo zaidi ya 40 vya wafuasi wake ambao aliwaagiza kufunga kula hadi kufa na miili yao kugunduliwa ilizikwa katika Shakahola Forest huko Kilifi.

Akizungumza wakati wa Gwaride la maafisa magereza Aprili 24, amesema mchungaji huyo alikuwa gaidi aliyewaamuru wakenya kufanya vitendo vilivyo kinyume na kanuni za Katiba

“Tunachokiona Kilifi, Shakahola ni sawa na ugaidi hakuna tofauti kati ya Mackenzie anayejifanya mchungaji na hali ni mhalifu wa kutisha na siku zote magaidi hutumia dini kuendeleza vitendo vyao viovu”

Pia ameagiza ofisi ya DCI Kenya  kuchunguza wachungaji wanaotumia dini kufanya vitendo viovu na kuwachukulia hatua ikiwemo kufungia makanisa yao.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags