Ruhusa kusafiri na mnyama wako kwenye ndege

Ruhusa kusafiri na mnyama wako kwenye ndege

Wakati asilimia kubwa ya mashirika ya usafiri wa angani yakipiga marufuku abiria kusafiri na wanyama, shirika la ndege la Marekani BARK Air, limeleta mapinduzi na sasa linamruhusu abiria kuweza kusafiri na wanyama wao.

Shirika hilo lilitoa taarifa hiyo siku ya jana Alhamis Mei 23, 2024 kupitia ukurasa wao wa Instagram huku lengo la kuchukua uamuzi huo likiwa ni kuhakikisha wanyama nao wanathaminiwa kwa kupanda ndege kama ilivyo kwa binadamu.

Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali nchini humo zimeeleza kuwa safari yake ya kwanza iliyofanyika April mwaka huu kutoka New York hadi Los Angeles iliuza tiketi kwa wingi huku abiria wakidaiwa kugharimu dola 6,000 sawa na Sh 15 milioni kwa safari za ndani na dola 8,000 sawa na Sh 20 milioni kwa safari za kimataifa.

Kwa sasa ndege hiyo inafanya safari zake New York City kupitia Uwanja wa Ndege wa Westchester County hadi Los Angeles kupitia Van Nuys na London kupitia Biggin Hill.

Kila safari ya ‘BARK Air’, inabeba mbwa au wanyama 15 na wamiliki wao ili kupata nafasi wakati wanyama hao wakati wa safari kuendelea kucheza na ku-enjoy wakiwa ndani ya ndege. Hata hivyo sharti kubwa la kupanda usafiri huo uwe umefikisha angalau miaka 18 hawaruhusu watoto.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags