Rose Ndauka:naacha muziki,movies rasmi

Rose Ndauka:naacha muziki,movies rasmi

Ebwana kutoka kwenye ukurasa wa instagram wa Star wa filamu nchini Rose Ndauka atangaza rasmi kuachana na Muziki pamoja na filamu yaani sanaa kiujumla.

Mimi Naureen Mkongwa maarufu kama Rose Ndauka, kwa ihari yangu mwenyewe leo natangaza rasmi kuacha kuigiza na kufanya Muziki rasmi mara baada ya kutoona faida na manufaa yake zaidi ya kudharauliwa kila kukicha na kushushiwa heshima yangu.

Kwakipindi kirefu sasa nimekuwa nikitumikia sanaa na ndio iliyonipa Umaarufu huu nilionao, nawashukuru sana Mashabiki zangu katika Tasnia ya Filamu lakini pia nawashukuru sana mashabiki wapya niliojizolea kwenye fani yangu nyingine ya Muziki kwa sapoti yenu pamoja ushauri mwingi na tofautitofauti mlionipatia.

Leo nimeamua rasmi kuachana na mambo yote yanayojihusisha na sanaa kutokana na dhulma, urimbukeni, ubabe, manyanyaso, ubadhilifu na mengine mengi yaliyojaa husda na chuki unapofanya vizuri.

Najua ntakuwa nimewakwaza wengi kutokana na maamuzi haya ila sina budi kutokana na kulinda heshima yangu niliyojijengea tangu naanza sana mpaka leo hii nipo kwenye ndoa na familia inayonitegemea kama mama.

Hakuna yoyote aliyenishawishi ila nimaamuzi yangu binafsi ambapo naamini kabisa mta yaheshimu na kuzingatia, Mume wangu mpenzi haffiyy najua ntakuwa nimekudisapointi sana juu ya maamuzi haya, ila naomba uyaheshimu kwa maslahi ya baadae ya watoto wetu.

Sanaa ya Bongo bila kujichachua kidogo, kuaa mtupu  ama kunyenyekea waliotangulia na mapapa fulani hivi huwezi kuwa bora, ndomana utakuta kila siku tunatoa watu walewale tu na uwezo wao fake, sasa kwasababu ya hawa haters kadhaa wanaochafua sanaa yetu nimeona nikae kimya.

Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki sanaa yetu kwa ujumla wake.

aisee niambie mdau kwa maoni yako hili alilolisema rose ndauka kamaanisha au kwa sababu leo ni siku ya wajinga duniani anatupima? dondosha comment yako hapo chini.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags