Ronaldo ashinda tuzo mfungaji bora 2023

Ronaldo ashinda tuzo mfungaji bora 2023

Nyota wa ‘klabu’ ya Al Nassr FC kutoka Saudi Arabia, Cristiano Ronaldo ameibuka kidedea kwa kushinda Tuzo ya Maradona kutoka Globe Soccer kama mfungaji bora kwa mwaka 2023 akiwa na magoli 54.

Ronaldo anakuwa mchezaji wa kwanza wa ‘timu’ ya #AlNassr kutwaa tuzo hiyo, ambapo mwaka 2022 tuzo ya Maradona ilichukuliwa na nyota wa ‘klabu’ ya #Barcelona Robert Lewandowski.

Ikumbukwe kuwa mwaka 2023 ulikuwa mzuri kwa Cristiano Ronaldo katika ‘soka’, wiki kadhaa zilizopita alipokea tuzo ya mfungaji bora duniani kutoka kwa (IFFHS) na tuzo ya mchezaji bora mwezi Disemba 2023 kutoka #SaudiProLeague






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags