Ronaldinho: Sitaangalia mechi yeyote Brazil

Ronaldinho: Sitaangalia mechi yeyote Brazil

Mwanasoka wa zamani Ronaldinho amedai kuwa hataishangilia wala kuangalia mechi yeyote ya Brazil kwenye fainali za Copa America kwa sababu amechoshwa na kipindi cha huzuni.

Akizungumza na Tovuti ya The New York Times Ronaldinho ambaye kwa sasa amestaafu soka amedai kuwa kwa sababu ya matokeo mabaya ni ngumu kwa sasa kutafuta morali ya kuangalia michezo hiyo na huenda hali hii ni kwa wote wanaopenda soka la Brazil.

Hata hivyo, amesema kuwa soka la Brazil haliridhishi katika miaka ya hivi karibuni akidai hakuna viongozi  ambao wanaheshimika kuongoza katika klabu zao zaidi ya kuwa na wachezaji wasio kuwa na viwango na ubora.

“Ndio hivyo, sitaangalia mechi yoyote ya Brazil kwenye Copa America wala kushangilia ushindi wowote. Nimechoshwa, ni kipindi cha huzuni kwa wote ambao wanalipenda soka la Brazil. Ni ngumu kwa sasa kutafuta morali ya kuangalia mechi zao.”

“Ni moja ya timu mbovu katika miaka ya hivi karibuni. Hakuna viongozi ambao wanaheshimika, zaidi ya kuwa na wachezaji wa kawaida tu.”

“Sijawahi kuona hali ikiwa mbaya kama hii, hawaheshimu jezi ya Brazil na hakuna soka la maana kabisa. Kiwango chetu kimekuwa moja ya kitu kibaya kuwahi kukishuhudia ni aibu.” - amesema nyota wa zamani wa.

Ikumbukwe kuwa gwiji huyo mwenye umri wa miaka 44 alistaafu soka mwaka 2018 na kuweka kumbukumbu ya rekodi zake nzuri katika baadhi ya vilabu ikiwemo Grêmio, Paris Saint-Germain, Barcelona, Milan, Flamengo, Querétaro, Fluminense na timu yake ya taifa ya Brazil.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags