Roboti wakwanza wa kiafrika kuzinduliwa leo Nigeria

Roboti wakwanza wa kiafrika kuzinduliwa leo Nigeria

Kundi la Makampuni ya Uniccon limesema linatazamia kuzindua roboti ya kwanza barani Afrika yenye sura ya binadamu inayoitwa ‘Omeife’, nchini Nigeria.

Mkurugenzi Mtendaji wa kikundi hicho, Bw. Chuks Ekwueme, ambaye alitangaza hayo katika taarifa yake jana mjini Abuja, alisema hafla hiyo itafanyika leo siku ya ijumaa.

Aidha Ekwueme alisema roboti huyo wa kike wa Kiafrika mwenye urefu wa futi sita anazungumza lugha kama huduma kwa biashara zinazohitaji kuunganisha watazamaji asilia wa Kiafrika, akiongeza kuwa ni roboti ya kazi nyingi na msaada.

Roboti hiyo inazungumza Kiingereza, Kifaransa, Kiarabu, na pia lugha za Kiafrika, kama vile Kiswahili, Pidgin, Wazobia, Afrikaans na Igbo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags