Rihanna: Nitavaa kawaida sana kwenye Met Gala

Rihanna: Nitavaa kawaida sana kwenye Met Gala

Ikiwa zimebaki siku chache tuu kuelekea tamasha la mitindo duniani lijulikanalo lijulikanalo kwa jina la ‘Met Gala’ mwanamuziki Rihanna amedai kuwa mwaka huu atavaa kawaida tofauti na miaka iliyopita.

Rihanna ameyasema hayo wakati akiwa kwenye moja ya mahojiano ambapo ameweka wazi kuwa mtoko wake wa mwaka huu hautakuwa kama miaka mingine kwani ameshakuwa mama hivyo hawezi kufanya vitendo alivyokuwa akivifanya katika tamasha hilo miaka ya nyuma.

Mashabiki wa msanii huyo kupitia mitandao ya kijamii wameendelea kuweka imani kwa Bad girl Ril kwani wanamjua jinsi gani hupendelea kutupia hivyo hata kama atavaa kawaida wanaamini atawafunika wote.

Met Gala au Met Ball, inatarajiwa kufanyika Jumatatu Mei 6, 2024 katika Ukumbi wa ‘Metropolitan Museum of Art’ Manhattan, New York City.
.
.
.
#MwanachiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags