Rihanna na Ayra Starr waonekana pamoja kwa mara nyingine

Rihanna na Ayra Starr waonekana pamoja kwa mara nyingine

Mkali wa Afrobeat kutoka Nigeria Ayra Starr ameendelea kushika vichwa vya habari baada ya kuonekana Rihanna wakiwa matembezi pamoja.

Kwa mujibu wa baadhi za tovuti zinaeleza kuwa mkali huyo wa ngoma ya ‘Diamond’ alimualika Ayra ili kusheherekea naye tamasha la kila mwaka lililofanyika katika mitaa ya Crop Over.

Kufuatia na video pamoja na picha za wawili hao wakiwa mmoja wa mtu wa karibu wa Rihanna alidai kuwa licha ya wawili hao kuhudhuria tamasha hilo pia walikutana tena kwa ajili ya kurekodi video ya ngoma yao mpya waliyoahidi kuifanya.

Hii itakuwa mara ya pili kwa Ayra Starr na Rihanna kukutana, utakumbuka kuwa April 17 mwaka huu walikutana kwa mara ya kwanza katika onesho la ‘Fenty X Puma’ lililofanyika jijini London.

Ambapo wawili hao walipata wasaa wa kuzungumza kwa mujibu wa vyombo vya habari mbalimbali nchini humo vimeeleza kuwa Riri alimuomba Ayra aingize verse kwenye moja ya ngoma zake.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags