Rayvanny atisha na chui truck tabora

Rayvanny atisha na chui truck tabora

Wanangu niaje? Kama kawaida katika burudani bhana mkali wa melody, Rayvanny a.k.a Chui atisha kwenye tamasha la muziki huko Tabora kwa aina yake ya performance.

Chui ameonyesha ubunifu wa hali ya juu katika tamasha la Fiesta huko Tabora kwa kuingia na Chui truck ikiwa na package yenye stage ambayo ina muonekano wa mazingira tofauti kama sitting room, bedroom na chumba chenye mvua.

TAZAMA CHUI TRUCK HAPA

Aisee! Rayvanny amekuwa akionyesha ubunifu tofauti tofauti katika mikoa ambayo tamasha hilo limepita, pia msanii huyo hakuwa ameperform katika tamasha hili kwa takribani miaka mitano, hii imethibitishia watu kwamba mwana ameamua kuwekeza katika kila show ya tamasha hilo kuonyesha utofauti na kuacha kumbukumbu katika vichwa vya mashabiki.

Chui kupitia ukurasa wake wa Instagram amepost video inayomuonesha akiperform kwenye Chui truck na kuandika ujumbe ukisema, “Ndoto yangu ilikua kufanya shows ambazo zitakua na utofauti kabisa na tulizozoea kila siku. Yaani inakua chumba, mara mvua inashuka, mara sitting room lakini muda huohuo ni jukwaa, imekula pesa nyingi sana lakini God is good, we did it.”

Dondosha comment yako hapo chini ubunifu wa Chui unaupa asilimia ngapi?






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Habiba Mohamed

A digital journalist and writer for mwananchi scoop My stories around entertainment,fashion, Artist profile, relationship, lifestyle and career.


Latest Post

Latest Tags