Rashford aing’anga’nia Man United

Rashford aing’anga’nia Man United

Imeripotiwa kuwa mshambuliaji wa klabu ya #ManchesterUnited Marcus Rashford, hana mpango wa kutaka kuondoka katika kikosi hicho msimu ujao na amedai kuwa atapinga endapo itatokea klabu hiyo kuwa na mpango wa kumuuza.

Licha ya kutokuwa na msimu mzuri klabuni hapo lakini ameonyesha kutokuwa na dalili za kuondoka kwenye kikosi hicho ambacho msimu huu kimekosa nafasi ya kufuzu ligi ya Mabingwa Ulaya  na kushindwa kuchukua kombe la Carabo.

Hata hivyo kumekuwa na tetesi kwamba mchezaji huyo raia wa Uingereza huenda atajiunga na timu ya Paris Saint-Germain FC ya Ufaransa.

Rashford alipandishwa katika kikosi cha kwanza cha Man United mwaka 2016, chini ya aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Louis van Gaal na mchezo wake wa kwanza kucheza kwenye Ligi Kuu England ilikuwa ni dhidi ya Arsenal ambapo alifunga mabao mawili na kutoa asisti moja.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags