Ramaphosa awaruhusu Wakenya kwenda South Africa bila kutumia VISA

Ramaphosa awaruhusu Wakenya kwenda South Africa bila kutumia VISA

Rais wa South Africa Cyrill Ramaphosa akiwa Nairobi, Kenya leo ametangaza kuwa kuanzia January 2023 Wakenya wataruhusiwa kwenda nchini South Africa bila kuhitajika kuwa na VISA kama ilivyo sasa.

Rais Ramaphosa ameyasema haya muda mfupi baada ya kufanya kikao na Rais William Ruto kwenye Ikulu ya Nairobi na kusema kuanzia hiyo January 2023 Wakenya wataruhusiwa kukaa nchini Afrika Kusini katika kipindi cha siku 90 ndani ya mwaka mmoja au kuingia na kutoka nchini humo zaidi ya mara moja kwa kuzingatia kutozidisha siku 90 katika vipindi hivyo tofauti tofauti ndani ya mwaka.

Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zinafaidika na makubaliano kama haya ya Raia wake kwenda South Africa bila VISA.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags