Ramaphosa akataa ombi la mazishi ya kitaifa kwa AKA

Ramaphosa akataa ombi la mazishi ya kitaifa kwa AKA

Waziri Mkuu wa Gauteng Panyaza Lesufi nchini Afrika Kusini alimuomba Rais Cyril Ramaphosa ruhusa ya kumpa rapa aliyeuawa Kiernan Forbes, maarufu kama AKA, mazishi ya kitaifa

Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa ombi la mazishi ya kiserikali kwa mwanamuziki maarufu wa Afrika Kusini aliyeuawa wiki iliyopita kwa kupigwa risasi limekataliwa na rais.

Panyaza alisema hakuomba fedha za serikali kwa ajili ya mazishi, bali jeneza lifunikwe bendera ya taifa na bendera kupeperushwa nusu mlingoti kwa heshima ya rapa huyo.

"Tulihisi kwamba mtu wa hadhi yake ya kimataifa, mtu wa hadhi ya kitaifa, lazima kuwe na aina fulani ya heshima, na tunataka kufafanua sio mchango wa kifedha," alisema Waziri Lesufi

Rapa huyo  anatarajiwa kupumzishwa katika nyumba yake ya milele(kuzikwa) siku ya Jumamosi ya tarehe 18, February.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post