Rais wa Barcelona ashitakiwa kwa rushwa

Rais wa Barcelona ashitakiwa kwa rushwa

Rais wa ‘klabu’ ya #Barcelona, Joan Laporta ashitakiwa kwa tuhuma za rushwa za kununua waamuzi wa ‘mechi’ kufuatia malipo yaliyofanywa kwenda kwa makampuni yanayohusishwa na aliyekuwa Makamu wa Rais wa kamati ya waamuzi, José María Enríquez Negreira.

Mashitaka hayo yanahusiana na awamu ya kwanza ya Laporta kuchaguliwa kama Rais wa ‘timu’ hiyo, kati ya 2003 na 2010. Hivyo, mashitaka ya madai ya rushwa yaliyowasilishwa dhidi ya ‘timu’ hiyo mwezi Septemba mwaka huu, yalitakiwa kuwakabili marais wa zamani, Josep María Bartomeu, Sandro Rosell, Negreira pamoja na mwanaye, Javier Enríquez Romero.

Hata hivyo, hakimu anayesimamia kesi hiyo aliamua kwamba, Laporta na bodi yake ya wakurugenzi waongezwe kwenye uchunguzi huo mpya kwani ni kesi endelevu inayohusisha awamu yake mpya.

Imeripotiwa kuwa Barcelona ilimlipa Negreira zaidi ya Euro 7 milioni zaidi ya tsh 18 bilioni ili aipendelee Barcelona, kati ya 2001 na 2018 alipokuwa Makamu wa Rais wa Kamati ya Waamuzi.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags