R.Kelly na uwezekano wa kubaki gerezani

R.Kelly na uwezekano wa kubaki gerezani

Muimbaji maarufu nchini Marekani R. Kelly anauwezekano wa kutotoka gerezani kwa mujibu wa Wakili wa Jimbo la Cook Kim Foxx aliwaambia waandishi wa habari kwamba ofisi yake inaamini "haki imetendeka" dhidi ya msanii huyo kwa makosa mawili. Kwahiyo R.Kelly anaangalia uwezekano wa kutotoka gerezani tena.”

Kwa mujibu wa taarifa nyingi zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari ni kuwa mwendesha mashtaka wa Illinois huko Chicago alifuta mashtaka kumi ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya msanii R Kelly huku gharama ilikuwa ni moja ya mambo yaliyopimwa katika uamuzi wake.

mwanamuziki huyo alipangiwa kufikishwa mahakamani Ijumaa katika kesi ya serikali, ambapo anatuhumiwa kuwanyanyasa kingono watu wanne, watatu kati yao wakiwa watoto wadogo. Kim alitangaza kesi dhidi ya Kelly mwaka wa 2019, akisema matukio hayo yalitokea kati ya Mei 1998 na Januari 2010. R.Kelly alikuwa anakabiliwa na kifungo cha miaka mitatu hadi saba kwa kila shtaka ikiwa atapatikana na hatia.

R.Kelly tayari anatumikia kifungo cha miaka 30 kwa tuhuma za ulaghai na biashara ya ngono baada ya kuhukumiwa huko New York mwaka jana, Mbali na hilo Kelly anastahili kuhukumiwa katika kesi ya pili ya shirikisho huko Chicago mwezi huu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags