Pope Odonwodo afariki dunia

Pope Odonwodo afariki dunia

Baada ya kuzuka sintofahamu kuhusiana na ajali aliyoipata Mwigizaji kutoka nchini Nigeria Pope Odonwodo hatimaye imethibitika kuwa mwigizaji huyo amefariki dunia saa chake baada ya kufikishwa hospitalini.

Taarifa ya kifo cha muigizaji huyo imetolewa na Rais wa Shirikisho la Waigizaji nchini Nigeria ambapo imeeleza kuwa hospitali mbili zimejaribu kupambana kumtibu mwingizaji huyo lakini imeshindikana.

Pope Odonwodo alifariki pamoja na watu wengine baada ya boti walilopanda kupinduka katika Mto Anam, ambapo imeripotiwa kuwa Pope alipanda kwenye boti hiyo kwa ajili ya matayarisho ya filamu yake mpya.

Video ya mwisho kuiposti kupitia ukurasa wake wa Instagram imemuonesha msanii huyo akiwa kwenye boti  alipopatia ajali iliyokuwa ikiambatana na ujumbe uliyokuwa ukieleza kuwa watu waone namna gani waigizaji huwa wanapitia wakati mgumu ili kutengeneza filamu bora kwa ajili ya kufurahisha mashabiki zake

Marehemu Pope ameacha mke na watoto watatu, amewahi kuonekana katika filamu mbalimbali zikiwemo ‘Okija & Pamela’, ‘Honey Money’, ‘No Way Through’, ‘Wrong Initiation’ na nyinginezo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags