Pogba afichua alivyotaka kustaafu mpira

Pogba afichua alivyotaka kustaafu mpira

Gwiji wa mpira duniani ambaye ni kiungo wa ‘klabu’ ya Juventus, Paul Pogba amekiri kuwa alifikiria kustaafu ‘soka’ kufuatia madai ya unyang’anyi yaliyohusisha familia yake.

 Kiungo huyo wa kimatafa kutoka Ufaransa alitishiwa na genge la watu wasiojulikana ambao walidaiwa kumlazimisha atoe mamilioni ya pesa huku kaka yake Mathias Pogba akihusishwa katika mpango huo.

Kaka wa mchezaji huyo alichunguzwa na polisi kutokana na madai hayo aliyohusishwa, akiwa mahabusu pamoja na watu wengine wanne kwa miezi mitatu mwaka jana.

Ingawa kaka huyo wa Pogba alikana shutuma hizo akidai hana hatia katika jaribio la unyang’nyi dhidi ya ndugu yake aliachiwa huru kufuatia amri ya mahakama huku akipigwa marufuku kuwasiliana na mdogo wake.

Kiungo huyo aliyewahi kubeba kombe la dunia mwaka 2018 aliripoti polisi kutoa ushahidi na kuzungumzia sakata hilo lilivyoathiri familia yake na kusema kuwa hatataka tena kucheza na alitaka kuwa mtu wa kawaida kwa lengo la watu wanao mzunguka wampende yeye na sio kwa sababu ya umaarufu wake.

Gwiji huyo aliwaambia polisi kwamba genge hilo la wahuni lilianza kumfatilia tangu Machi mwaka jana.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags