PETE AONGEZA WALINZI BAADA YA VITISHO VYA KANYE

PETE AONGEZA WALINZI BAADA YA VITISHO VYA KANYE

Kufuatia vitisho vinavyotolewa na msanii maarufu nchini Marekani Kanye West kwenda kwa Pete Davidson ambaye ni mpenzi wa Kim Kardashian, imeripotiwa kuwa Pete ameamua kuongeza walinzi wa kumlinda.

Pete ambaye ni mchekeshaji maarufu huko Marekani ameamua kuongeza walinzi binafsi kufuatia vitisho alivyovisikia kwenye ngoma mpya ya Kanye West na The Game unaojulikana kwa jina la ‘Eazy’.

Hata hivyo imeelezwa kuwa Pete atakuwa akitumia walinzi wa Kim wakati wakiwa pamoja katika mizunguko mbalimbali.

Unaambiwa katika ngoma hiyo, Kanye amesikika akiimba “God Saved me from that crash, just so I can beat Pete Davidson.”






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags