Pep aipa Arsenal ubingwa

Pep aipa Arsenal ubingwa

Imeripotiwa kuwa kocha wa klabu ya #ManchesterCity, #PepGuardiola amesisitiza kuwa klabu ya #Arsenal ina nafasi kubwaya kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu ikiwa wao wataangusha pointi katika mechi moja kati ya tatu zilizosalia.

Man City ambayo haijafungwa kwenye mechi 20 mfululizo imeendeleza  rekodi hiyo wikiendi iliyopita baada ya kushinda mabao 5-1 dhidi ya timu ya  Wolves ambapo nyota  wao Erling Haaland alifunga mabao manne.

Kwa sasa kikosi hicho cha Guardiola kipo katika nafasi ya pili nyuma ya Arsenal wanao ongoza kwa pointi zao 83 ikiwa ni tofauti ya pointi moja dhidi yao lakini Man City ina faida yakuwa na mchezo mmoja mkononi.

Hivyo mechi tatu zilizosalia kwa Man City itacheza dhidi ya Fulham, Tottenham na West Ham wakati Arsenal mbili zilizosalia itakutana na Man United na Everton.

.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags