Pazia Sauti za Busara 2025 lafunguliwa

Pazia Sauti za Busara 2025 lafunguliwa

Hatimaye pazia la tamasha la muziki Sauti za Busara 2025, limefunguliwa leo Februari 14,2025, Ngome Kongwe, Stone Town kisiwani Unguja na Journey Ramadhan ambaye ni Mtendaji Mkuu wa tamasha hilo

Akizungumza wakati wa ufunguzi huo Journey amesema kauli mbiu ya mwaka huu ni kupaza sauti kwa ajili ya amani duniani. Hiyo ikiwa ni kutokana machafuko ambayo yametokea ulimwenguni.

"Nina ujumbe mdogo kuhusu kwanini tuliamua kuchagua kauli mbiu hii kwa mwaka huu. Katika dunia ambayo migogoro inatisha. Kila mmoja wetu ana nguvu ya kuwa sauti ya amani.

"Hii si tu kuhusu kupinga ukosefu wa haki. Pia ni kuhusu kuhamasisha majadiliano, kuunda nafasi ya kuelewana na kujenga uhusiano kati ya watu wa aina mbalimbali. Amani ya kweli inaanza tunapozungumza kwa huruma na kusikiliza kwa hisia, tukithamini hadithi na mtazamo wa kila mtu,"amesema

Hata hivyo ameongezea kuwa kupitia muziki ni rahisi kupaza sauti kupitia jumbe zinazotolewa.

"Tumeshuhudia migogoro mingi Afrika, kama ninavyosema. Tuache muziki uzungumze kwa sababu sauti za amani zinanza leo hadi tarehe 16 Februari,"amesema






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags