Paula, Marioo Waonesha Sura Ya Mtoto Wao

Paula, Marioo Waonesha Sura Ya Mtoto Wao

Mwanamuziki Marioo ambaye anatamba na wimbo wa ‘Tete’ na mpenzi wake Paula Kajala wameonesha sura ya mtoto wao Amarah kwa mara ya kwanza.

Ikiwa leo ni siku ya kuzaliwa ya Mtoto huyo wawili hao wamefichua sura ya mtoto wao huku wakimtakia kheri katika siku yake ya kuzaliwa.

“Leo natabasamu kwa sababu mwaka mmoja uliopita, moyo wangu ulizaliwa tena. Wewe ni mtoto wangu wa kwanza, zawadi ya maisha yangu, na sababu ya kila maombi yangu. Kila siku nawe ni somo, ni furaha, ni baraka.


Happy 1st birthday my love! Umenigeuza kuwa mama mwenye nguvu, uvumilivu na upendo wa kweli. Nitakupenda, kukulinda na kukuombea hadi pumzi yangu ya mwisho. You made me a mother, and that changed everything,” ameandika Paula

Ikumbukwe siku chache zilizopita Paula na Marioo walitangaza kufanya sherehe kubwa ya mtoto wako kutimiza mwaka mmojq, sherehe ambayo itahudhuriwa na mastaa mbalimbali kutoka Bongo akiwemo Billnass, Nandy, Wolper, na wengineo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags