Papa Francis amewaonya makasisi na watawa kuhusu hatari ya kutazama video ama picha za ngono (ponografia) mtandaoni akisema "inadhoofisha moyo wa kipadre".
Papa, mwenye umri wa miaka 86, alikuwa akijibu swali kuhusu jinsi vyombo vya habari vya kidijitali na kijamii vinapaswa kutumiwa vyema, katika kikao kilichofanyika Vatican.
Ponografia, alisema, ilikuwa "tabia ambayo watu wengi wanayo... hata makasisi na watawa". "Ibilisi huingia kutoka huko," Papa aliwaambia makasisi na waseminari.
Kuhusu jinsi ya kuvinjari katika mitandao ya kijamii na ulimwengu wa kidijitali, alisema ni lazima zitumike lakini akawaambia wasipoteze muda mwingi kuzitumia.
"Moyo safi, ambao Yesu anapokea kila siku, hauwezi kupokea habari hizi za ponografia," alisema.
Aliwashauri "futa (picha na video za ngono) kutoka kwa simu yako, ili usiwe na majaribu mkononi".
Mafundisho ya kanisa huona ponografia kama kosa dhidi ya usafi wa maadili.
Matatizo ya afya ya akili yanayoweza kusababishwa na kutazama picha za ngono
Ukiacha imani tafiti zinaonesha kwamba kutazama ponografia pekee kunapunguza msongo wa mawazo na kuchanganyikiwa.
Lakini, mara kwa mara kuangalia ponografia, hiyo yenyewe ina matokeo mabaya.
Pia huongeza msongo wa mawazo.
Kutazama Ponografia kupita kiasi kunaweza kusababisha matatizo katika ndoa. Kukatishwa tamaa hutokea kati ya wanandoa wakati akili inapoanza kutarajia mifumo ya kufikirika, isiyowezekana ya ngono.
Leave a Reply