Panya avamia uwanja wa Man City

Panya avamia uwanja wa Man City

Kwenye mchezo kati ya ‘klabu’ ya #ManchesterCity na ‘klabu’ ya #Sheffield jana Jumamosi, panya mmoja aliingia uwanjani (eneo la kuchezea) na kusimamisha kwa muda shughuli za maandalizi ya uwanja wa #Etihad, kwa ajili ya kipindi cha pili.

Kwa mujibu wa #SkySports, panya huyo aliingia uwanjani wakati wa mapumziko na alitembea hadi kwenye benchi la ufundi la Man City, huku akiwapa kazi wahudumu wa uwanja huo kumtafuta na kumtoa.

Mchezo huo ulimalizika kwa Man City kupata ushindi wa mabao 2-0 na sasa ‘klabu’ hiyo imerudisha matumaini kwenye harakati za kutetea taji lao la Ligi Kuu England baada ya kutoka kushinda kombe la dunia la ‘klabu’ nchini Saudia Arabia.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags