Otile Brown: Usishindane na Watu kwenye Mitandao

Otile Brown: Usishindane na Watu kwenye Mitandao

Basi bwana kwenye pita pita zetu huko mjini Instagram Mwanamuziki maarufu kutoka Nchini Kenya Otile Brown kupitia instastory yake ameamua kufunguka mazito na kueleza kuwa achana na mitandao inakupotezea muda.

“maisha yana viwango ishi kwenye kiwango chako utajikuta unakuwa, maana itakupa Amani na Amani itakupa furaha, itakutuliza na ukitulia utafanya maamuzi sahihi bila ushawishi wa kutaka kushindana na watu kwenye mitandao  na ukawekeza pesa zako kwa vitu vya msingi na utajikuta unafanikiwa bila ya kutumia nguvu nyingi” ameandika Otile Brown

Aidha mwanamuziki huyo liendelea kwa kufunguka mambo ya msingi na kusema kuwa “utajili upo akilini jaribu kutafuta utulivu na furaha kwa hicho kidogo ndio pale unajaaliwa uwe tayari ki akili kuyamudu, Baraka za mwenyezi mungu punguza strees za mitandao, wengi ni matajiri, wasio na hela wengi huenda umewazidi  wengi miradi yao ni kukupotosha tu so amkaa” ameandika Otile Brown

Aloooooh! Ni maneno konki sana haya wewe mfuatiliaji wa Mwananchi Scoop je unakubaliana na maneno ya mwanamuziki huyu au tukuache kidogo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags