Ommy Dimpoz: Sijaoga toka Ronaldo anishike bega

Ommy Dimpoz: Sijaoga toka Ronaldo anishike bega

Hahahhaha! Make hapa kwanza ncheke, inabidi na sie wengine twende tukapige picha hata na Messi ili tupate pa kutambia maana toka kijana Dimpoz apige picha na kupostiwa katika ukurasa wa manchester united amekuwa akitutesa sana na kutamba sana katika mitandao yake yote ya kijamii.

Basi bwana kauli hiyo ya yeye kutooga ameitoa kupitia instastory yake ikiambatana na video ambayo yuko na mchezaji wa yanga Mayele na kusema kuwa “ yani sijaoga toka anishike bega, na hili bega sio tu Ronaldo ameligusa yaani hadi Mayele kama nawaona mnavyokelekwa” amesema Ommy Dimpoz

Duuuuuuuuh! Jamani jamani kijana anajua kuwatesa wasanii wenzake mana anatamba yeye tu katika mitandao ya kijamii, embu dondosha picha yako nawewe mwanangu sana ukiwa na star yoyote ili uweze kuwatambia.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags