Ommy Dimpoz: Namba ya mganga wa Haji ninayo

Ommy Dimpoz: Namba ya mganga wa Haji ninayo

Duuuuuuh! Huyu bwana harusi wa jana bwana anaendelea kuzua balaa katika mitandao ya kijamii haswa kwa baadhi ya wasanii kutaka kufanya na kuwa na ujasiri kama aliokuwa nao  Bugati kwa kuongeza mke.

Basi bwana kwa yule kijana alietusumbuaga sana kuhusiana na kupiga picha na mchezaji maarufu wa nje Ronaldo, Ommy dimpoz kupitia instastory yake nae amefunguka na kuandika kuwa, “Wanawake mnaolalamika hamjaolewa namba ya mganga wa Haji Manara ninayo mimi mnione, yaani wallah nikikuwa nataka kuwa kama Haji maana haogopi kwenye kufanya maamuzi,” ameandika Ommy Dimpoz.

Haya haya wakutaka kuolewa mnaitwa huku kuna ujumbe wenu kutoka kwa Ommy mwenye Dimpoz zake mjini.

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags