Nyoshi El Saadat ataka bongo fleva waimbe live

Nyoshi El Saadat ataka bongo fleva waimbe live

Mwanamuziki nyota wa muziki wa dansi, anayemiliki bendi ya Bogoss Musica, Nyoshi El Saadat amewashauri wasanii wa Bongo Fleva kujikita zaidi katika kuimba muziki wa mubashara (live) ili kuwapa raha mashabiki wao.

Mtunzi huyo na mwimbaji wa bendi ya Bogoss aliliambia Mwanaspoti wasanii wanatakiwa kuujua muziki na kupiga ala mbalimbali na kuimba laivu badala ya kuishia kuwa waimbaji tu ambao kila mtu anaweza kufanya.

“Nitoe ushauri kwa wasanii wa Bongo Fleva, wasiache kujifunza kutoka kwa wenzao kama Alikiba na Barnaba, ukiwatazama wakiwa jukwaani unaona kabisa wanajua wanachokifanya hadi unafurahia kusikiliza anachokiimba. Wapo wasanii wanaojitahidi kuimba vizuri wawapo jukwaani kama Alikiba, Mbosso na Jaydee," alisema Nyoshi.

Alisema msanii ukijua kupiga tumba, magitaa na ala nyingine itawasaidia zaidi kutumbuiza kwa aina ya 'Live band' na hata malipo yataongezeka zaidi, kwani kuna mashabiki hasa wa kigeni wanapenda mtindo huo.

Nyoshi aligusia wanamuziki wa Kikongo wamekuwa wakifanya vizuri kwa upande wa kupiga muziki wa mubashara (Live band) kutokana na kujikita kwao kujifunza vyombo mbalimbali vya kimuziki.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags