Nusu ya watanzania wanatumia internet kila siku

Nusu ya watanzania wanatumia internet kila siku

Ripoti ya robo mwaka unaoishia Machi 2023 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inaonyesha kuwa zaidi ya nusu ya watanzania wanatumia huduma ya intaneti huku mtandao wa Facebook ukiongoza kwa matumizi makubwa ya bando.

Ripoti hiyo inayoonyesha mwenendo wa sekta ya mawasiliano nchini kwa kipindi cha Januari, Februari na Machi inaonyesha hadi Machi 2023 Watanzania milioni 33 walikuwa wanatumia huduma za intaneti ambayo ni sawa na asilimia 53.4 ya Watanzania wote.

Aidha idadi hiyo ya watumiaji wa intaneti imeongezeka kwa asilimia 48 hadi Machi 2023 ikilinganishwa na idadi ya mwaka 2018 iliyokuwa watu milioni 22.3.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags