Njia za kumfanya mkeo au mpenzi wako akupende zaidi

Njia za kumfanya mkeo au mpenzi wako akupende zaidi

Aloooooooh! It’s another furahi day mtu wangu wa nguvu sasa leo katika mahusiano kama kawaida yetu tuko na mada Atari kabisa ambazo zitakusaidia katika mahusiano yako, wewe mwanaume ulie katika ndoa yako inabidi kuzingatia haya ili uweze kudumu katika maisha yako ya ndoa.

Ndoa yenye afya na furaha husitawi kwa kujitolea, subira, na mambo muhimu zaidi pamoja na furaha Mke wako ndiye mwenzi wako wa roho na mwenzi wako wa maisha. Anafanya maisha yako kuwa ya furaha kwa kutunza mahitaji yako na kukusaidia kila hatua ya njia zote unazopitia.

Kumfurahisha mkeo sio kazi ngumu Utashangaa jinsi mabadiliko rahisi yanaweza kufanya maajabu katika uhusiano wako na kumfanya afurahi siku nzima.

Uwe msikilizaji mzuri

Wakati fulani mke wako anahitaji kuzungumza nawewe inabidi ukae na utulie ili umskilize kwa umakina pia jitahidi sana kumtia moyo kwa kumwambia yote yatakuwa sawa. Pia mskilize bila hukumu, mkumbatie, na umwambie kwamba uko kwa ajili yake.

Jua nini anataka/anapenda

Makini na kile mke wako anapenda kifungua kinywa kitandani, Au labda anataka tu uweke kiti ili muweze kukaa pamoja na kuanza kupiga story pamoja. Kufanya vitendo vile vidogo kunaweza pia kumfanya ahisi kama unamuelewa zaidi na kumpenda pia.

Mkumbatie mara kwa mara

Iwe unapotoka kwendaa kazini au kurudi hakikisha unamkumbatia kwa nguvu mwenzawako kwa kumuonyesha upendo wako na shukrani kwa kila jambo alilokufanyia, mguso wa kimwili na ishara zinaweza kwenda mbali na kumbusu ni ishara mojawapo ya kumuonyesha unampenda.

Mpongeze

Kumpongeza ni njia nzuri ya nkuongeza kujiamini, mpongeze kwa mafanikio, mwonekano, ujuzi na yote yanayomfanya kuwa maalum, usifanye hivyo tu ukiwa karibu bali pia hata mbele ya wafanyakazi wenzake marafiki jamaa wake wa karibupia , itasaidia kuonyesha kuwa hauogopi kuwajulisha watu wengi jinsi unavyompenda.

Mpikie

Kumpikia mwenzawako ni njia ambayo itamfanya ajiskie mtu maalum wa thamani na mwenye furaha muda wote, unaweza kupika chakula anachokipenda Zaidi, hii itamfanya aamini kuwa wewe ni mwanaume watofauti kushinda wengine, jitihada zako ndo zitamfanya aongeze mapenzi na kukupenda daima.

Mwamini

Mashaka na mawazo ya uongo huunda vizuizi visivyo vya lazima katika uhusiano kwa hivyo maneno ambayo huna ushahidi nayo, pia epuka Zaidi kuskiliza maneno ya watu yaani maneno ya kimbea hii itasaidia Zaidi kwake kujua kuwa unamuami na unaamini anachokwambia.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags