Njia nzuri za kupongezana kazini

Njia nzuri za kupongezana kazini

Mambo vipi!! Siku zote bwana wahenga wanasema kazi na dawa, kama kawaida yetu sisi tumeapa kukutumikia wewe msomaji wetu wa Mwanachi Scoop na kukupatia mastory yatakayo kujuza mambo mbalimbali kuhusu maisha, kazi, burudani, michezo, afya na yale yanayojiri vyuoni.

Hivi ulishawa kufanya utu kwa mtu halfu akasifia kitu ulicho kifanya, ulijisikiaje kwa wakati ulee jamani kuna ki vibe Fulani hivi sasa kama hauna kawaida anza kufanya hivyo hasa makazini.

Leo katika segment ya kazi nimekuja na mada ambayo itakufanya ujifunze jambo furani kuhusiana na maisha ya kazini, kama tunavyojua bwana kazini kuna mambo mengi ya kuudhi lakini kwa upande mwingine kuna yanayofurahisha pia.

Siku zote ukienda katika mkuisanyiko wa watu wengi kila mmoja anavile atakavyo kuchukulia, huenda ukawa na bosi anayekupongeza zaidi kuwahi kutokea, lakini hiyo haimaanishi kwamba unapaswa kumwacha akupe heshima zote wewe inabidi nawewe uwape heshima wafanyakazi wenzako.

Ukifanikiwa kufanya jambo kama hili utaeneza upendo na kuongeza tija ya kila mtu. Ikiwa wasimamizi wako hawana wakati  au mwelekeo wa kutoa pongezi ofisini, inaweza kuwa juu yako kuunda mazingira ya kazi ambayo ya afya na shukrani.

Tunacho kizungumza hapa ni kuepuka kuwa mbinafsi na watu ili wasikuone hivyo basi unatakiwa kufanya mambo ambayo yatawafanya wafanyazi wenzio waamini kuwa upo pamoja nao.

Na haya ndo mambo/njia nzuri za kupongezana kazini… 

Kutoa mialiko, eg chakula nk

Jenga uhusiano na wafanya kazi wenzio kwa kuwakaribisha chakula ili waondoe dhana ya kukuona mbinafsi, andaa tafrija uliyotayarisha nyumbani ili kuwashukuru wafanyakazi wenza kwa usaidizi wao hata kama hawajakusaidia ilimradi tuu ujiweke karibu nao.

Hata kama sio nyumbani unaweza siku moja moja kuwatoa na mkaenda kula sehemu za mgahawa au kuwaletea bahasha ya chokoleti/ice cream iliyowekwa kwenye meza yake ya kufanyia kazi na kwa karibisha kwa upendo na ikiwa mfanyakazi mwenzako amejitolea kukusaidia, mualike hata lunch kama ishara ya kushukuru kwa kile alicho kutendea . 

Kuandika dokezo/ kutuma kadi za pongezi


Ingawa kumsifu mwenzako ana kwa ana daima kunafaa na sio watu wengi wanafata utaratibu huo, nenda hatua zaidi na uandike maneno yako. Je, umevutiwa na wasilisho ambalo mfanyakazi mwenzako alilofanya ambalo alilipata katika kampuni wateja watano wapya? Mtumie mfanya kazi mwenzio barua pepe ukimwambia hivyo.

Weka wasambazaji wa kadi za kumbukumbu na uzitumie kuandika maelezo ya shukrani au maneno ya kutia moyo na sifa usipuuze mitandao ya kijamii ujumbe kwenye  imeli ya mwenzako unaosema, “Ninavutiwa na ujuzi wako!" baada ya kufanya mauzo makubwa inaweza kuleta tabasamu usoni mwake.

Unapotumia mitandao ya kijamii, kumbuka kuwa wateja wanaweza pia kufikia akaunti yake, kwa hivyo usitoe maelezo yanayohusiana na kazi.

Omba Ushauri

Njia moja bora ya kumsifu mtu ni kumwomba ushauri hii inamjulisha kuwa hauthamini kazi yake tu bali pia unaamini kwamba ana kitu cha kukupa. Na ushauri hapa pendelea kumuomba unaohusiana na maswala ya kazi na sio ya familia kwasababu hakuna kuaminiana kazini katika kuambiana maswala ya familia, mahusiano nk.

Kuwa na tabia ya kuwapongeza wanaofanya vizuri katika kazi

Sio tu kumwambia mfanyakazi mwenzako jinsi alivyo na thamani kwako, pia unafanya kazi ili kutangaza thamani yake kwa watu wengine unaweza kusema,

"John niliogopa kwamba ripoti ingechelewa baada ya kuwa na matatizo mengi ya kupanga picha siwezi kuamini kuwa umeipata kwa wakati" Kugeukia wengine katika chumba na kusema, "Yeye kabisa ameweza” italeta husiano mzuri kwa wafanya kazi wengine hata kwenye vitabu ya dini vina sema kuwa muombe mwenzako mema huwenda wewe ukapata zaidi.

Kuwapa train ya jambo fulani

Kama tunavyojua kila siku kunazuka mitindo mipya ya utendaji wa kazi kitechnolojia so unaweza kuwaelekeza wafanyakazi wenzio kwa kile ulicho kigundua hupelekea kupata sifa na kufanya kazi kwa muda mrefu bila kuchoka na kwa sababu unahitajika zaidi hapo kazi sio tu na bosi wako hata wafanya kazi wenzio wanapenda uwepo wako uendelee hapo kazini.

Ukiwasaidia kuwaelekeza katika jambo la kiofisi hii itakuja kuwasaidia baadae, endapo taasisi itakapo chukua jukumu kupunguza wafanyakazi ili kuondokana na mzigo wa uendeshaji, mfanyakazi mbunifu hubaki kutokana alichojifunza kupitia kwako.

Kutenda jambo jema kwa mtu haitokani nawewe awe amekutendea jambo jema pia, kitu utakacho muelekeza mwenzio leo na kikaja kumfanya afanikiwe baada litakuwa ni jambo la kutokukusahau maisha yake yote.

Kazini ni mahali ambapo mtu huishi kila siku so jitahidi sana kuishi vizuri na wenzio, maana siku hizi wana msemo wao kuwa huwezi jua mbeleni nani atakutoa kimaisha, jitahidini kupendana, kuheshimiana na kujaliana mkiwa kazini.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags