Njia mbadala za kujisomea na kujifunza kupitia “Smartphone” yako

Njia mbadala za kujisomea na kujifunza kupitia “Smartphone” yako

 

Vijana wengi wanatamani kujifunza vitu mbalimbali, inaweza aidha kuwa kuongeza maarifa ili kuelewa zaidi walichofundishwa darasani au kujifunza vitu vipya. Ukiachana na kufunzwa darasani, kuna njia nyingine nyingi tu ambazo unaweza kuzitumia kuongeza ujuzi na maarifa, hadi ukafikia hatua ya kuweza kubobea katika kile utakacho kifanya, baadhi ya njia mbadala za kujisomea na kujifunza kupitia smartphone yako ni kama ifuatavyo:

 

  • YOUTUBE

YouTube ni moja kati ya mitandao maarufu zaidi duniani, ambapo unaweza kupata mafunzo kwa mfumo wa video. Kupitia mtandao huo, unaweza kujifunza namna ya kuongeza ujuzi, kama vile kujifunza kutengeneza programu, elimu ya biashara na kadhalika. Ukiingia kwenye mtandao huo, kwenye alama ya tafuta, kila unachotaka kusoma na zitatokea video mbalimbali vyenye kufundisha ujuzi husika.

 

  • GOOGLE

Google ni chanzo kingine kizuri sana cha kujifunzia. Unaweza ukaitumia kujua kuhusiana na suala lolote lile na utakutana na tovuti mbalimbali zinazofundisha ujuzi unaotaka kujua. Vilevile Google hutoa kozi maalumu kwaajili ya taaluma mbalimbali, ambapo zipo za bure na za kulipia. Tumia fursa hii kujifunza na kujinyakulia cheti cha mafunzo, kitakacho kusaidia baadaYe.

 

  • KUSOMA KOZI MITANDAONI

Njia nyingine ya kujifunzia ni kusoma kozi mitandaoni. Tovuti nyingi hutoa kozi maalumu kwaajili ya kitu fulani, mfano: kozi za mauzo ya kidigitali, kozi za mawasiliano ya umma na mengineyo. Mfano wa baadhi ya tovuti ni Coursera, Masterclass na Udemy.

 

  • KUSOMA VITABU MITANDAONI

Unaweza pia ukasoma vitabu mbalimbali mitandaoni kulingana na kile unachotaka kujifunza. Vitabu mbalimbali vyenye lengo la kukusaidia wewe kujifunza ujuzi fulani, kujiendeleza kimaisha na hata kuongeza maarifa. Unaweza ukapakua baadhi ya vitabu bure mtandanoni, au kuvinunua kupitia tovuti kama vile Amazon na kuzisoma kupitia Kindle au iBooks.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post