Njia 5 za kupunguza unene bila diet wala mazoezi

Njia 5 za kupunguza unene bila diet wala mazoezi

Inawezekana kupunguza uzito bila kufanya mazoezi wala diet, ndio inawezekana kama utaamua kufuata njia 5 zifuatazo ambazo nimekuandalia leo

  1. Pakua chakula kwenye sahani ndogo

Siku zote elewa kuwa sahani kubwa ya chakula itafunya utake kujza chakula kingi bila sabbau maalum il I kuweza kushinda jaribu hilo hakikisha unapochukua chakula weka kweny sahani ndogo na ubongo wako utadhani umeweka chakula kingi.

Tafiti zinaonesha kuwa sahani kubwa zinafanya watu waone wamepakua chakula kidogo kwa sababu ya nafasi kubwa hivyo kuwafanya wapakue zaidi.

  1. Kula taratibu na tafuna chakula vizuri

Kutafuna chakula ipasavyo kunakufanya ule taratibu hivyo kupelekea kushiba haraka. Ubongo wako unahitaji muda ili kutambua kwamba umeshiba.

Tafiti zinaonesha kwamba watu wanaokula haraka sana wana uwezekano mkubwa zaidi wa kuongezeka uzito ukilinganisha na watu wanaokula taratibu.

Ukiwa makini unaweza kugundua kuwa watu wengi wenye uzito uliopindukia huwa wanakula haraka sana. Kwahiyo kama ungependa kupunguza uzito basi anza leo kujijengea tabia ya kula taratibu.

  1. Kula vyakula vyenye nyuzi nyuzi (Fibre)

Ulaji wa vyakula vyenye fibre husaidia kupunguza kasi ya mmeng’enyo wa chakula tumboni ivyo kukufanya ujisikie umeshiba kwa muda mrefu.

Mfano wa vyakula vyenye nyuzi nyuzi ni kunde, maharage, nafasa zote zilizokobolewa, viazi vitamu pamoja na mboga za majani.

  1. Kunywa maji mara kwa mara

Unywaji wa maji nusu lita dakika 30 kabla ya kila mlo kwa mtu mzima husaidia kupunguza njaa na kiasi cha chakula kitakacholiwa.

  1. Acha kula vinywaji vyenye sukari

Ukichukua hatua ya kuacha kunywa vinywaji vyenye sukari kama soda, energy grinks na juice basi wewe upo katika hatua nzuri ya kupungua uzito.

Unywaji wa vinywaji vya sukari kama soda unahusishwa na kusaababisha au kuzidisha magonjwa mengi mwilini ikiwamo Kisukari.

Bia pia zinaunganishwa kwenye kundi hilo kwa sababu zinatengenezwa na chakula cenye asili ya wanha ambayo ni sawa sawa na sukari.

Juice ya matunda pia zinajumuishwa kwa sababu zinaweza kuwa na sukari, niwakumbushe tu Sukari ikiwepo nyingi mwilini hufanya hormone inayofanya mafuta yayeyushwe kupungua.

Hivyo basi kama unakula na kunywa vitu vyenye sukari nyingi ni ngumu kuyeyusha mafuta  na kupunguza uzito wa mwili wako.

Ili kuepuka kunywa vinjwaji hivyo unashauliwa kunywa maji kwa wingi, chai au kahawa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post