Nicki Minaj asimama na Wizkid

Nicki Minaj asimama na Wizkid

Mwanamuziki wa Marekani Nicki Minaj ameeleza kuwa wimbo wa mkali wa Afrobeat Wizkid ‘Essence’ unastahili kushinda tuzo ya Grammy kutokana na ubora wake.

Rapa huyo ambaye amewahi kutamba na ngoma ya ‘Super Bass’ amefunguka kuwa kutokana na ubora wa ngoma hiyo inastahili kupata tuzo ya Grammy.

Nicki alisema Essence ulikuwa wimbo bora wa mwaka mzima, ukishika namba za juu kwenye chati za muziki za Billboard tangu alipotoka mwaka 2021, huku ukipata dili mbalimbali.

“Tunapaswa kuwa na bodi yetu wenyewe ya Grammy kwa sababu wimbo wa Wizkid wa ‘Essence’ unapaswa kushinda kipengele cha Best Global Music Performance.” alisema Nicki Minaj.

Ngoma ya ‘Essence’ ambayo Wizkid alimshirikisha Tems ilitoka miaka mitatu iliyopita huku mpaka kufikia sasa una zaidi ya watazamaji milioni 198 katika mtandao wa Youtube






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags