Nicki Minaj amtia moyo Lil Wayne

Nicki Minaj amtia moyo Lil Wayne

‘Rapa’ Nicki Minaj ameshiriki maneno ya kutia moyo kwa mwanamuziki Lil Wayne baada ya msanii huyo kutochaguliwa kwenye onesho la ‘Super Bowl Halftime’ 2025.

Nicki kupitia ukurasa wake wa Instagram alifunguka kuwa hana hisia mbaya kwa Kendrick Lamar kuchagulia kufanya show hiyo huku akimtia moyo Lil kwa kumtaka awe mtulivu kwani hata hili litapita.

“Hii nayo itapita, lakini kile ulichokifanya kwa utamaduni wa Hip Hop kitabaki. Hili ni jaribu la wakati, Mara nyingi jaribio letu kubwa na la kudhalilisha ni njia tu ya Mungu kupata utukufu. Walikutumia tuu siku zote watu waovu wanatumia pesa kusambaza mabaya yako lakini Bwnaa atafuta kila jaribio na si tu litawarudia, bali litarudishwa jingine bora zaidi ya hilo,” ameandika Nicki.

Utakumbuka kuwa mapema wiki iliyoisha waandaji wa tamasha la ‘Super Bowl Halftim’ walimtaja ‘rapa’ Kendrick Lamar kuwa atatumbuiza katika onesho hilo jambo ambalo halikumpendeza Wayne na baadhi ya mashabiki kwani walihisi kuwa msanii huyo angechaguliwa kwa sababu yeye ndio msanii aliyezaliwa katika mji wa New Orleans.

Super Bowl Halftime 2025 inatarajia kufanyika Februari 9, 2025 huko jijini New Orleans nchini Marekani.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags