Nicki Minaj aachia kionjo kolabo yake na Wizkid

Nicki Minaj aachia kionjo kolabo yake na Wizkid

Mwanamuziki wa Marekani Nicki Minaj amecheza kionjo cha nyimbo aliyorekodi na mkali wa Afrobeat kutoka Nigeria Wizkid.

Minaj ameshare kionjo cha ngoma hizo wakati alipokuwa live Instagram huku akiweka wazi kuwa wimbo huo walirekodi na Wizkid miaka nane iliyopita pamoja na nyingine walizorekodi miaka mitano iliyopita.

Mbali na kushare ngoma hiyo ambayo haijatoka hadi leo, Nicki alieleza kuwa anamkubali sana Wizkid kwa sababu anautu, upendo na heshima kubwa.

Hata hivyo alifunguka siku ya kwanza kukutana na msanii huyo ambapo alidai kuwa walikutana studio New York alipokuwa akirekodi album yake ya ‘Queen’ ya mwaka 2018.

Wizkid sio msanii wa kwanza kutoka Nigeria kufanya ‘kolabo’ na Nicki kwani Februari mwaka huu ‘rapa’ Minaj pia aliachia kionjo cha ngoma yake na msanii Burna Boy.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags