Nguo za Yeezy gap zadaiwa kuibiwa

Nguo za Yeezy gap zadaiwa kuibiwa

‘Timu’ ya wafanyakazi katika kampuni ya mwanamuziki Kanye West, Ye’s imeripoti kuwa zaidi ya nguo zenye thamani ya dola 1 milioni zimeibiwa kwenye ghala la nguo la kampuni hiyo lililoko Las Angeles nchini Marekani.

Taarifa hiyo imetolewa na mkuu wa wafanyakazi kampuni ya Ye’s Milo Yiannopoulos, ambapo aliiambia Tmz kuwa wafanyakazi waligundua kiasi kikubwa cha nguo za ‘Yeezy GAP’ kwenye ghala la Ye's zilipotea siku chache zilizopita ambapo wamedai kuwa takribani nguo 60,000 zimeibia, zenye thamani ya dola 1.2 milioni.

Aidha Yiannopoulos alieleza kuwa ‘timu’ yake ya wafanyakazi haikujua nguo hizo zilikwenda wapo, lakini waligundua kuwa zimeibiwa baada ya kuona akaunti ya shabiki wa Kanye akiuza nguo hizo za Yeezy GAP kwa dola 20.

Hata hivyo Yiannopoulos amedai kuwa tayari wamemtambua mmoja wa wezi waliuhusika katika wizi huo hivyo atashirikiana na polisi kwa ajili ya uchunguzi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags