Ngoma iliyomleta mjini marehemu Costa Titch yazidi kukimbiza Youtube

Ngoma iliyomleta mjini marehemu Costa Titch yazidi kukimbiza Youtube

Wimbo wa marehemu mwanamuziki kutoka Afrika Kusini Costa Titch wa ‘Big Flexa’ umeendelea kukimbiza kupitia mtandao wa YouTube ambapo kwa sasa umeripotiwa kufikisha zaidi ya watazamaji milioni 100.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa msanii huyo ambao unasimamiwa na mama yake mzazi alitoa shukrani kwa kundi la ‘Titch Gang’ kuendeleza urithi huo.

“Shukrani za pekee kwa AlfaKat, Miss Pammie , Ma Gang na timu nzima kwa kutimiza ndoto hii, najua Costa anajivunia kila mmoja wenu Nawashukuru ‘Titch Gang’ kwa kudumisha urithi wake naona kabisa hii inahitaji sherehe, endelea kufuatilia tuna matangazo mengi ya kusisimua njiani ya kuweka historia kwa pamoja (Mama Titch)”

Ikumbukwe kuwa mwamuziki huyo alifariki March 11 mwaka jana baada ya kupata mshtuko na kudondoka akiwa jukwaani alipokuwa akitumbuiza katika tamasha la ‘Utra Music’ nchini Africa Kusini, na sababu ya kifo chake ikiwekwa wazi na familia yake Mie 2024 kuwa Costa Titch alipata mgandamizo mkubwa katika moyo wake.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags