Neymar kutolewa Brazil

Neymar kutolewa Brazil

Inadaiwa kuwa mchezaji wa #Al Hilal aliyesajiliwa hivi karibuni #Neymar ni majeruhi licha ya kuhusishwa katika kikosi Brazil kwa ajili mchezo dhidi ya Peru na Bolivia, hiyo ni baada ya ‘Kocha’ wa ‘timu’ hiyo #JorgeJesus kufichua siri kuwa mchezaji huyo ana majeraha na hatakuwa ‘fiti’ kucheza ‘mechi’ ya kimataifa akiwa na kikosi cha ‘timu’ ya taifa ya #Brazili mwezi ujao.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Jesus ambaye ndiyo kwanza ameanza kibarua baada ya kuteuliwa amethibitisha kuwa Neymar ni majeruhi.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alikuwa nje ya dimba kuanzia February mwaka huu kufuatia upasuaji wa kifundo cha mguu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags