Neymar kuondoka PSG, Chelsea yatajwa

Neymar kuondoka PSG, Chelsea yatajwa

Mshambuliaji wa PSG anadaiwa  huenda akajiunga na Chelsea katika dirisha la usajili lililofunguliwa mwezi wa saba na linatarajiwa kufungwa mwezi huu, baada ya kuibuka kwa taarifa ya kuwa ameomba kuondoka PSG.

Neymar ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2025, anadaiwa kuwasilisha barua ya kuomba kuondoka PSG, siku chache zilizopita kwa kile kinachoelezwa anahitaji changamoto mpya. 

Moja kati ya ‘timu’ ambazo zinadaiwa kutaka kuipata huduma ya fundi huyu wa Brazil ni Chelsea ambayo bado inapambana kuboresha eneo lao la ushambuliaji.

Moja ya sababu inayodaiwa kumnyima furaha Neymar, ni kitendo cha mashabiki wa timu hiyo kuonyesha wazi kuwa hawamtaki baada ya mapema mwaka huu kukusanyika nje ya nyumba yake wakiwa na mabango ya kumtaka aondoke kwenye team hiyo.

Neymar alijiunga na PSG akitokea Barcelona mwaka 2017 kwa ada ya uhamisho iliyovunja rekodi na kumfanya awe mchezaji ghali zaidi Duniani hadi sasa ambayo ilikuwa ni Pauni 198 milioni.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags